Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un
Habari zilizotufikia muda si mrefu ni kwamba Mufti Mkuu wa Tanzania Shekh Issa Shabani Simba Amefariki dunia, leo asubuhi.
Mufti Shekh Issa Shabani Simba, alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya Kisukari kwa muda mrefu kidogo. Kabla ya kufariki, Marehemu Muft Simba alikuwa amelazwa kwenye Hospitali ya TMJ Mikocheni na alikuwa amefanyiwa operasheni ndogo kabla ya umauti kumkuta.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, Mazishi ya Mufti Simba yatafanyika leo baada ya Swalat dhuhr shambani kwake uko Kigamboni.
Kwa wale wote watakaopata nafasi basi wanaweza kuudhuria Msibani nyumbani kwake Mikocheni, jijini Dar es Salaam.
--DUA'A
Ewe Mwenyezi Mungu hakika Issa Shabani Simba yuko katika dhima yako na kamba ya ujirani wako, basi mkinge na fitina ya kaburi na adhabu ya moto nawe ndiwe mstahiki wa utekelezaji na ukweli, basi msamehe na umrehemu hakika Wewe ni mwingi wa kusamehe, mwingi wa kurehemu.